Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Tulisema, “Shukeni kutoka Peponi nyote! Na utawajia, nyinyi na vizazi vyenu vinavyofuatia, ujumbe wenye mambo ya kuwaongoza kwenye haki. Wenye kuufuata huo kwa vitendo, hawatakuwa na hofu kuhusu mustakbala wao wa Akhera, wala hawatakuwa na huzuni juu ya vitu walivyovikosa vya ulimwenguni.