Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Baqarah 2:74

2:74
ثم قست قلوبكم من بعد ذالك فهي كالحجارة او اشد قسوة وان من الحجارة لما يتفجر منه الانهار وان منها لما يشقق فيخرج منه الماء وان منها لما يهبط من خشية الله وما الله بغافل عما تعملون ٧٤
ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِىَ كَٱلْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةًۭ ۚ وَإِنَّ مِنَ ٱلْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ ٱلْمَآءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ ٱللَّهِ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ٧٤
ثُمَّ
قَسَتۡ
قُلُوبُكُم
مِّنۢ
بَعۡدِ
ذَٰلِكَ
فَهِيَ
كَٱلۡحِجَارَةِ
أَوۡ
أَشَدُّ
قَسۡوَةٗۚ
وَإِنَّ
مِنَ
ٱلۡحِجَارَةِ
لَمَا
يَتَفَجَّرُ
مِنۡهُ
ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ
وَإِنَّ
مِنۡهَا
لَمَا
يَشَّقَّقُ
فَيَخۡرُجُ
مِنۡهُ
ٱلۡمَآءُۚ
وَإِنَّ
مِنۡهَا
لَمَا
يَهۡبِطُ
مِنۡ
خَشۡيَةِ
ٱللَّهِۗ
وَمَا
ٱللَّهُ
بِغَٰفِلٍ
عَمَّا
تَعۡمَلُونَ
٧٤
Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yafanya. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Lakini nyinyi hamkufaidika na hilo. Kwani baada ya miujiza yote hii yenye kupita mipaka ya uwezo wa kiumbe, nyoyo zenu zilikuwa ngumu na shupavu kwa namna ambayo hakuna kheri iliopenyeza ndani, na hazikulainika mbele ya miujiza yenye kushinda niliyowaonesha, mpaka nyoyo zenu zikafikia hadi ya kuwa ni kama jiwe gumu, bali zililishinda jiwe kwa ugumu wake. Kwani miongoni mwa mawe kuna yanayopanuka na kutoboka na maji yakabubujika kwa wingi kutoka humo mpaka yakawa ni mito yenye kupata. Na miongoni mwayo kuna yanayofanya nyufa, yakapasuka na kuchimbuka maji ya chemchemi na mikondo. Na miongoni mwayo kuna yanayoanguka kutoka juu ya milima kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kumuadhimisha. Na Mwenyezi Mungu Hakuwa ni Mwenye kughafilika kwa mnayoyafanya.