Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Baqarah 2:76

2:76
واذا لقوا الذين امنوا قالوا امنا واذا خلا بعضهم الى بعض قالوا اتحدثونهم بما فتح الله عليكم ليحاجوكم به عند ربكم افلا تعقلون ٧٦
وَإِذَا لَقُوا۟ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍۢ قَالُوٓا۟ أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ ٱللَّهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَآجُّوكُم بِهِۦ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ٧٦
وَإِذَا
لَقُواْ
ٱلَّذِينَ
ءَامَنُواْ
قَالُوٓاْ
ءَامَنَّا
وَإِذَا
خَلَا
بَعۡضُهُمۡ
إِلَىٰ
بَعۡضٖ
قَالُوٓاْ
أَتُحَدِّثُونَهُم
بِمَا
فَتَحَ
ٱللَّهُ
عَلَيۡكُمۡ
لِيُحَآجُّوكُم
بِهِۦ
عِندَ
رَبِّكُمۡۚ
أَفَلَا
تَعۡقِلُونَ
٧٦
Na wanapo kutana na wale walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Mnawaambia aliyo kufunulieni Mwenyezi Mungu ili wapate kukuhojieni mbele ya Mola wenu Mlezi? Basi hamfahamu nyinyi? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Hawa Mayahudi, wakikutana na Waumina, wanasema kwa ndimi zao, “Tumeamini dini yenu na Mtume wenu aliyebashiriwa katika Taurati.” Na wakiwa faragha, wao kwa wao, hawa wanafiki wa kiyahudi, huwa wakiambiana kwa njia ya kukemeana, “Vipi nyinyi mnawahadithia Waumini yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewabainishia katika Taurati kuhusu Muhammad, mkawapa hoja juu yenu mbele ya Mola wenu Siku ya Kiyama? Kwani hamfahamu mkajihadhari?”