Na wako miongoni mwao wasio jua kusoma; hawakijui Kitabu isipo kuwa uwongo wanao utamani, nao hawana ila ni kudhania tu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kati yao kuna watu wasiojua kusoma na kuandika, na wasioijua Taurati na yaliyomo ndani yake ya sifa za Nabii na Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na hawana chochote kuhusu hayo isipokuwa ni maneno ya urongo na dhana mbovu.