Watayapata humo wayatakayo daima dawamu. Hii ni ahadi juu ya Mola wako Mlezi, inayo ombwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Hawa wenye utiifu watavipata wanavyovitamani vya ladha za neema, starehe yao humo ni ya daima, na kuingia kwao humo ilikuwa ni ahadi ya Mola wako, ewe Mtume, yenye kuombwa, kwa kuwa waja wema wa Mwenyezi Mungu wanamuomba (hiyo Pepo). Na Mwenyezi Mungu Haendi kinyume na ahadi Yake.