Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Hajj 22:58

22:58
والذين هاجروا في سبيل الله ثم قتلوا او ماتوا ليرزقنهم الله رزقا حسنا وان الله لهو خير الرازقين ٥٨
وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ قُتِلُوٓا۟ أَوْ مَاتُوا۟ لَيَرْزُقَنَّهُمُ ٱللَّهُ رِزْقًا حَسَنًۭا ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ ٥٨
وَٱلَّذِينَ
هَاجَرُواْ
فِي
سَبِيلِ
ٱللَّهِ
ثُمَّ
قُتِلُوٓاْ
أَوۡ
مَاتُواْ
لَيَرۡزُقَنَّهُمُ
ٱللَّهُ
رِزۡقًا
حَسَنٗاۚ
وَإِنَّ
ٱللَّهَ
لَهُوَ
خَيۡرُ
ٱلرَّٰزِقِينَ
٥٨
Na walio hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha wakauwawa au wakafa, bila ya shaka Mwenyezi Mungu atawaruzuku riziki njema. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wanao ruzuku. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wale waliyotoka majumbani mwao kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kuinusuru Dini Yake, yoyote kati yao atakayeuawa akiwa katika hali ya kupigana na makafiri, na yoyote kati yao atakayekufa bila kupigana, Mwenyezi Mungu Atawaruzuku Pepo na starehe zake zisizokatika wala kuondoka. Na kwa hakika, Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Mbora wa wenye kuruzuku.