Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
074

Al-Muddaththir 74:22 ثم عبس وبسر ٢٢

74:22
ثُمَّ
عَبَسَ
وَبَسَرَ
٢٢
Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Kisha akafinya uso wake na akazidi katika hali ile ya ukunjaji uso kwa kukosa hila za kufanya na kutopata ila yoyote ya kuitia dosari Qur’ani.
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 74, Ukurasa 576, Juzuu 29

8. Basi litapo pulizwa barugumu, 9. Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu. 10. Kwa makafiri haitakuwa nyepesi. 11. Niache peke yangu na niliye muumba; 12. Na nikamjaalia awe na mali mengi, 13. Na wana wanao onekana, 14. Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa. 15. Kisha anatumai nimzidishie! 16. Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu! 17. Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana. 18. Kwani hakika yeye alifikiri na akapima. 19. Basi ameangamia! Vipi alivyo pima! 20. Tena ameangamia! Vipi alivyo pima! 21. Kisha akatazama, 22. Kisha akakunja kipaji, na akanuna. 23. Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari. 24. Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa. 25. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu. 26. Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. 27. Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? 28. Haubakishi wala hausazi. 29. Unababua ngozi iwe nyeusi. 30. Juu yake wapo kumi na tisa. 31. Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia