Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapo fika ajali yake; na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wala Mwenyezi Mungu hatoichelewesha nafsi yoyote utakapokuja wakati wa kifo chake na umri wake ukakoma. Na Mwenyezi Mungu, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake, ni mtambuzi wa yale mnayoyatenda: mema na mabaya, na Awetawalipa nyinyi kwa hayo.