Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Munaafiqun 63:4

63:4
۞ واذا رايتهم تعجبك اجسامهم وان يقولوا تسمع لقولهم كانهم خشب مسندة يحسبون كل صيحة عليهم هم العدو فاحذرهم قاتلهم الله انى يوفكون ٤
۞ وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا۟ تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌۭ مُّسَنَّدَةٌۭ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ ٱلْعَدُوُّ فَٱحْذَرْهُمْ ۚ قَـٰتَلَهُمُ ٱللَّهُ ۖ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ٤
۞ وَإِذَا
رَأَيۡتَهُمۡ
تُعۡجِبُكَ
أَجۡسَامُهُمۡۖ
وَإِن
يَقُولُواْ
تَسۡمَعۡ
لِقَوۡلِهِمۡۖ
كَأَنَّهُمۡ
خُشُبٞ
مُّسَنَّدَةٞۖ
يَحۡسَبُونَ
كُلَّ
صَيۡحَةٍ
عَلَيۡهِمۡۚ
هُمُ
ٱلۡعَدُوُّ
فَٱحۡذَرۡهُمۡۚ
قَٰتَلَهُمُ
ٱللَّهُۖ
أَنَّىٰ
يُؤۡفَكُونَ
٤
Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na unapowatazama wanafiki hawa, yanakufurahisha maumbile yao na mandhari yao, na wanapozungumza unayasikiliza mazungumzo yao kwa ufasaha wa ndimi zao, na hali wao kutokamana na utupu wa nyoyo zao kuwa hazina Imani na akili zao kuwa hazina fahamu wala elimu yenye manufaa, ni kama vigogo vilivyotegemezwa kwenye ukuta, visivyokuwa na uhai.wanadhania kila sauti ya ukelele inawashukia wao na ina madhara kwao kwa kujua kwao uhakika wa hali yao na uoga wao mwingi na hofu iliyojikita nyoyoni mwao. Wao ndio maadui wa kikwelikweli wenye uadui mwingi kwako wewe na kwa Waumini. Basi jichunge na wao, Mwenyezi Mungu Amewadhalilisha wao na Amewatoa kwenye rehema Yake. Basi ni vipi wao wanaiepuka haki na wanaelekea kwenye yale ambayo wao wamo ndani yake ya unafiki na upotevu.