Sawa sawa kwao, ukiwatakia maghfira au hukuwatakia maghfira, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yanalingana kwa wanafiki hawa, uwaombee msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ewe Mtume, au usiwaombee, kwani Mwenyezi Mungu Hatazisamehe dhambi zao kabisa kwa sababu ya kuendelea kwao na uasi na kujikita kwao kwenye ukafiri. Hakika Mwenyezi Mungu Hawaelekezi kwenye Imani watu wanaomkanusha waliotoka nje ya utiifu Kwake.