Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
023

Al-Muuminun 23:66 قد كانت اياتي تتلى عليكم فكنتم على اعقابكم تنكصون ٦٦

23:66
قَدۡ
كَانَتۡ
ءَايَٰتِي
تُتۡلَىٰ
عَلَيۡكُمۡ
فَكُنتُمۡ
عَلَىٰٓ
أَعۡقَٰبِكُمۡ
تَنكِصُونَ
٦٦
Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu, 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

«Zilikuwa aya za Qur’ani zikisomwa kwenu, ili mupate kuziamini, na mlikuwa mnazikimbia hamtaki kuzisikia na kuzikubali na kuzitumia, kama anavyofanya mwenye kurudi nyuma kwa kule kurudi kwake nyuma.
«Zilikuwa aya za Qur’ani zikisomwa kwenu, ili mupate kuziamini, na mlikuwa mnazikimbia hamtaki kuzisikia na kuzikubali na kuzitumia, kama anavyofanya …
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 23, Ukurasa 346, Juzuu 18

62. Na hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa. 63. Lakini nyoyo zao zimeghafilika na hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyo vifanya. 64. Hata tutakapo watia katika adhabu wale walio dekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watapo yayatika. 65. Msiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi. 66. Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu, 67. Na huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau. 68. Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia yasiyo wafikia baba zao wa zamani? 69. Au hawakumjua Mtume wao, ndio maana wanamkataa? 70. Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki. 71. Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao. 72. Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanao ruzuku. 73. Na kwa yakini wewe unawaita kwenye Njia Iliyo Nyooka. 74. Na hakika wale wasio iamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo. 75. Na lau tungeli warehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo bila ya shaka wangeli endelea katika upotofu wao vile vile, wakitangatanga. 76. Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea. 77. Mpaka tulipo wafungulia mlango wa adhabu kali, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia