Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
054

Al-Qamar 54:48 يوم يسحبون في النار على وجوههم ذوقوا مس سقر ٤٨

54:48
يَوۡمَ
يُسۡحَبُونَ
فِي
ٱلنَّارِ
عَلَىٰ
وُجُوهِهِمۡ
ذُوقُواْ
مَسَّ
سَقَرَ
٤٨
Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu! 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Siku watakapokokotwa ndani ya Moto kwa nyuso zao na waambiwe, «Onjeni ukali wa adhabu ya moto wa Jahanamu.»
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 54, Ukurasa 530, Juzuu 27

41. Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni. 42. Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza. 43. Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani? 44. Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu. 45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma. 46. Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi. 47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu. 48. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu! 49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo. 50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho. 51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka? 52. Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni. 53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa. 54. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito. 55. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia