Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Al-Qasas 28:60

28:60
وما اوتيتم من شيء فمتاع الحياة الدنيا وزينتها وما عند الله خير وابقى افلا تعقلون ٦٠
وَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَىْءٍۢ فَمَتَـٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيْرٌۭ وَأَبْقَىٰٓ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ٦٠
وَمَآ
أُوتِيتُم
مِّن
شَيۡءٖ
فَمَتَٰعُ
ٱلۡحَيَوٰةِ
ٱلدُّنۡيَا
وَزِينَتُهَاۚ
وَمَا
عِندَ
ٱللَّهِ
خَيۡرٞ
وَأَبۡقَىٰٓۚ
أَفَلَا
تَعۡقِلُونَ
٦٠
Na chochote mlicho pewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayo baki zaidi. Basi je, hamfahamu? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na chochote kile mlichopewa, enyi watu, cha mali na watoto, basi hayo ni starehe ya nyinyi kustarehe nayo katika maisha haya ya kilimwengu na ni pambo la kujipamba nalo. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu, yaliyowekewa watu walio watiifu Kwake na wenye kumtegemea, ni bora zaidi na ni yenye kusalia zaidi, kwani hayo ni ya daima yasiyomalizika. Basi nyinyi hamuwi na akili, enyi watu, ya kuzingatia kwayo, mkajua lema na ovu?