Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiihimize. Ametakasika na Ametukuka na wanayo mshirikisha nayo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kumekaribia kusimama Kiyama na kutoka amri ya Mwenyezi Mungu ya kuwaadhibu nyinyi, enyi makafiri, basi msiifanyie haraka adhabu kwa njia ya kuicheza shere ahadi ya Mtume kwenu. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameepukana na ushirika na washirikina.