Kwa hayo Yeye anaizalisha kwa ajili yenu mimea, na mizaituni,na mitende, na mizabibu, na kila namna ya matunda. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanao fikiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Anawatolea nyinyi kutoka kwenye ardhi, kwa maji haya mamoja, mazao mbalimbali: Anawatolea nyinyi kwayo mizaituni, mitende na mizabibu, na anawatolea nyinyi kwayo kila aina ya matunda, makubwa kwa madogo. Hakika katika hayo pana ushahidi waziwazi kwa watu wanaofikiri na wakazingatia.