Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
016

An-Nahl 16:54 ثم اذا كشف الضر عنكم اذا فريق منكم بربهم يشركون ٥٤

16:54
ثُمَّ
إِذَا
كَشَفَ
ٱلضُّرَّ
عَنكُمۡ
إِذَا
فَرِيقٞ
مِّنكُم
بِرَبِّهِمۡ
يُشۡرِكُونَ
٥٤
Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi, 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Kisha Anapowaondolea matatizo na magonjwa, kitahamaki linatoka kundi la watu miongoni mwenu wakawa wanawafanya asiyekuwa Yeye kuwa ni washirika pamoja na Yeye na wategemewa.
Kisha Anapowaondolea matatizo na magonjwa, kitahamaki linatoka kundi la watu miongoni mwenu wakawa wanawafanya asiyekuwa Yeye kuwa ni washirika pamoja…
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 16, Ukurasa 272, Juzuu 14

51. Na Mwenyezi Mungu amesema: Msiwe na miungu wawili! Hakika Yeye ni Mungu Mmoja. Basi niogopeni Mimi tu! 52. Na ni vyake Yeye viliomo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je! Mtamcha mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu? 53. Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakikuguseni madhara mnamyayatikia Yeye. 54. Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi, 55. Wakizikataa neema tulizo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua! 56. Na hao ambao hata hawawajui wanawawekea sehemu ya tunavyo waruzuku.Wallahi! Bila ya shaka mtasailiwa kwa hayo mliyo kuwa mnayazua! 57. Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu, Aliyetakasika! Na wao wenyewe, ati ndio wawe na hayo wanayo yatamani! 58. Na mmoja wao akibashiriwa kwa msichana, uso wake unasawijika,naye kajaa chuki. 59. Anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa aliyo bashiriwa! Je,akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama uovu wa wanavyohukumu! 60. Hali ya wasio iamini Akhera ni ovu; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia