Na hatukukuteremshia Kitabu isipo kuwa uwabainishie yale ambayo wanakhitalifiana, na kiwe Uwongofu na Rehema kwa watu wanao amini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hatukukuteremshia Qur’ani, ewe Mtume, isipokuwa ni uwafunulie watu wazi yale ambayo walikuwa wakitafautiana juu yake, ya dini na hukumu, ili hoja zisimame kwao kwa maelezo yako ambayo hayauachii upotofu njia ya kuingia nyoyoni. Na kwa kuwa Qur’ani ni uongofu, haitoi nafasi ya kutunduwaa, nayo ni rehema kwa Waumini katika kufuata kwao uongofu na kujiepusha kwao na upotevu.