Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: An-Nahl 16:69

16:69
ثم كلي من كل الثمرات فاسلكي سبل ربك ذللا يخرج من بطونها شراب مختلف الوانه فيه شفاء للناس ان في ذالك لاية لقوم يتفكرون ٦٩
ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ فَٱسْلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًۭا ۚ يَخْرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌۭ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَٰنُهُۥ فِيهِ شِفَآءٌۭ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةًۭ لِّقَوْمٍۢ يَتَفَكَّرُونَ ٦٩
ثُمَّ
كُلِي
مِن
كُلِّ
ٱلثَّمَرَٰتِ
فَٱسۡلُكِي
سُبُلَ
رَبِّكِ
ذُلُلٗاۚ
يَخۡرُجُ
مِنۢ
بُطُونِهَا
شَرَابٞ
مُّخۡتَلِفٌ
أَلۡوَٰنُهُۥ
فِيهِ
شِفَآءٞ
لِّلنَّاسِۚ
إِنَّ
فِي
ذَٰلِكَ
لَأٓيَةٗ
لِّقَوۡمٖ
يَتَفَكَّرُونَ
٦٩
Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizo fanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina matibabu kwa wanaadamu.Hakika katika haya ipo Ishara kwa watu wanao fikiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kisha kuleni katika kila tunda mnalolipenda na mzifuate njia za Mola wenu mlizotayarishiwa ili kutafuta riziki majabalini na kati ya miti. Na Mwenyezi Mungu Amewasahilishia njia hizo, hamupotei katika kurudi hata kama ni mbali. Inatoka kwenye matumbo ya nyuke asali yenye rangi tafauti: nyeupe, manjano, nyekundu na nyiginezo. Na kwenye hiyo asali pana tiba ya magonjwa ya watu. Hakika katika hayo wanayoyafanya nyuki pana ushahidi wenye nguvu juu ya uweza wa Muumba wao kwa watu wanaofikiria na wakazingatia.