Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
053

An-Najm 53:35 اعنده علم الغيب فهو يرى ٣٥

53:35
أَعِندَهُۥ
عِلۡمُ
ٱلۡغَيۡبِ
فَهُوَ
يَرَىٰٓ
٣٥
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Je huyu anayekata kheri yake ya kutoa ana ujuzi wa ghaibu kuwa yeye atamalizikiwa na mali yaliyoko mkononi mwake ndipo akaizuia kheri yake asiitoe, na akawa aliona hilo waziwazi? Mambo si hivyo! Hakika ni kwamba yeye aliacha kutoa sadaka na kufanya kheri, kutenda wema na kuunga kizazi kwa ubahili na…
Je huyu anayekata kheri yake ya kutoa ana ujuzi wa ghaibu kuwa yeye atamalizikiwa na mali yaliyoko mkononi mwake ndipo akaizuia kheri yake asiitoe, na…
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 53, Ukurasa 527, Juzuu 27

33. Je! Umemwona yule aliye geuka? 34. Na akatoa kidogo, kisha akajizuia? 35. Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? 36. Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa? 37. Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi? 38. Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine? 39. Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe? 40. Na kwamba vitendo vyake vitaonekana? 41. Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu. 42. Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho. 43. Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio. 44. Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha. 45. Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike 46. Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa. 47. Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine. 48. Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha. 49. Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra. 50. Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza, 51. Na Thamudi hakuwabakisha, 52. Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi; 53. Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua. 54. Vikaifunika vilivyo funika. 55. Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka? 56. Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani. 57. Kiyama kimekaribia! 58. Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu. 59. Je! Mnayastaajabia maneno haya? 60. Na mnacheka, wala hamlii? 61. Nanyi mmeghafilika? 62. Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia