Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na Mwenyezi Mungu Peke Yake wanamsujudia, wakinyenyekea na kufuata, walioko mbinguni na ardhini wote, Waumini wanamsujudia na kumnyenyekea kwa ridhaa na hiari, na makafiri wanamnyenyekea kwa nguvu, kwa kuwa wao wanafanya kiburi kumuabudu na hali yao na maumbile yao yanawakanusha juu ya hilo. Na vivuli vya viumbe vinafuata utukufu wa Mwenyezi Mungu, vinatembea kulingana na matakwa Yake mwanzo wa mchana na mwisho wake.