Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mwenyezi Mungu Anakifuta Akitakacho miongoni mwa hukumu na mengineyo, na Anakiacha kisalie Akitakacho miongoni mwa hizo kwa hekima fulani Anayoijua. Na Kwake kuna asili ya Kitabu, nacho ni Al-Lawh„ Al-Mah,fūd,: Ubao uliohifadhiwa ambao yamethibitishwa ndani yake kimaandishi hali za viumbe mpaka Siku ya Kiyama.