Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
037

As-Saaffat 37:29 قالوا بل لم تكونوا مومنين ٢٩

37:29
قَالُواْ
بَل
لَّمۡ
تَكُونُواْ
مُؤۡمِنِينَ
٢٩
Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Hapo watasema wafuatwa kuwaabia wafuasi, «Mambo si kama vile mnavyodai, bali ni nyoyo zenu zilikuwa zimekataa kuamini, zimeuelekea ukafiri na uasi.
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 37, Ukurasa 447, Juzuu 23

22. Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu. 23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu! 24. Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa: 25. Mna nini? Mbona hamsaidiani? 26. Bali hii leo, watasalimu amri. 27. Watakabiliana wao kwa wao kuulizana. 28. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia. 29. Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini. 30. Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu. 31. Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu. 32. Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu. 33. Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja. 34. Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu. 35. Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna. 36. Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu? 37. Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume. 38. Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu. 39. Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia