Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kuna neema nyingine kwenu, enyi Waumini, mtaipenda, nayo ni msaada kutoka kwa mwenyezi Mungu utakaowajia na ushindi wa haraka utakaopatikana mikononi mwenu. Na wape bishara Waumini, ewe Mtume, ya kunusuriwa na kupata ushindi duniani na kupata Pepo kesho Akhera.