Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi na adui zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo na akamfanya kuwa ana washirika wa kuabudiwa, na hali yeye anaitwa aingie kwenye Uislamu na kumpwekesha Mwenyezi Mungu Peke Yake kwa ibada. Na Mwenyezi Mungu Hawaafikii, wale waliozidhulumu nafsi zao kwa kukufuru na kukanusha, kwenye njia ambayo ndani yake kuna kufaulu kwao