Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu wenye kukanusha kufufuliwa wamesema, «Je, itakapokuwa mchanga nyama yetu na mifupa yetu, je, tutafufuliwa tuwe umbo lingine?» huku wakiona kuwa hilo liko mbali kutokea na huku hawataki kuifikia haki. Na hilo kwao ni udhalimu na ushindani, hii ni kwamba wao wanakanusha kukutana na Mola wao Siku ya Kiyama.