Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: As-Sajdah 32:27

32:27
اولم يروا انا نسوق الماء الى الارض الجرز فنخرج به زرعا تاكل منه انعامهم وانفسهم افلا يبصرون ٢٧
أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا نَسُوقُ ٱلْمَآءَ إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلْجُرُزِ فَنُخْرِجُ بِهِۦ زَرْعًۭا تَأْكُلُ مِنْهُ أَنْعَـٰمُهُمْ وَأَنفُسُهُمْ ۖ أَفَلَا يُبْصِرُونَ ٢٧
أَوَلَمۡ
يَرَوۡاْ
أَنَّا
نَسُوقُ
ٱلۡمَآءَ
إِلَى
ٱلۡأَرۡضِ
ٱلۡجُرُزِ
فَنُخۡرِجُ
بِهِۦ
زَرۡعٗا
تَأۡكُلُ
مِنۡهُ
أَنۡعَٰمُهُمۡ
وَأَنفُسُهُمۡۚ
أَفَلَا
يُبۡصِرُونَ
٢٧
Je! Hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa mimea wanayo kula wanyama wao na wao wenyewe? Je! Hawaoni? 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwani hawakuona wenye kukanusha kufufuliwa baada ya kufa kwamba sisi tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu iliyo ngumu ambayo haina mimea, tukatoa kwa maji hayo mimea yenye rangi mbalimbali yenye kuliwa na wanyama wao na miili yao ikapata chakula cha kuwafanya wao waishi kwayo? Kwani hawazioni neema hizi kwa macho yao wakajua kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwahuisha wafu na kuwafufua kutoka makaburini mwao?