Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
026

Ash-Shuaraa 26:119 فانجيناه ومن معه في الفلك المشحون ١١٩

26:119
فَأَنجَيۡنَٰهُ
وَمَن
مَّعَهُۥ
فِي
ٱلۡفُلۡكِ
ٱلۡمَشۡحُونِ
١١٩
Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Basi tukamuokoa na wale walio pamoja na yeye katika jahazi iliyojazwa aina mbalimabali za viumbe alivyovibeba pamoja na yeye.
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 26, Ukurasa 372, Juzuu 19

105. Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume. 106. Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?. 107. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. 108. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 109. Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 110. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. 111. Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini?. 112. Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?. 113. Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!. 114. Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. 115. Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri. 116. Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. 117. Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. 118. Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. 119. Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. 120. Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia. 121. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 122. Kina A'd waliwakanusha Mitume.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia