Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ash-Shuura 42:20

42:20
من كان يريد حرث الاخرة نزد له في حرثه ومن كان يريد حرث الدنيا نوته منها وما له في الاخرة من نصيب ٢٠
مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ ٱلْـَٔاخِرَةِ نَزِدْ لَهُۥ فِى حَرْثِهِۦ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ ٱلدُّنْيَا نُؤْتِهِۦ مِنْهَا وَمَا لَهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ ٢٠
مَن
كَانَ
يُرِيدُ
حَرۡثَ
ٱلۡأٓخِرَةِ
نَزِدۡ
لَهُۥ
فِي
حَرۡثِهِۦۖ
وَمَن
كَانَ
يُرِيدُ
حَرۡثَ
ٱلدُّنۡيَا
نُؤۡتِهِۦ
مِنۡهَا
وَمَا
لَهُۥ
فِي
ٱلۡأٓخِرَةِ
مِن
نَّصِيبٍ
٢٠
Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Yoyote Anayetaka kwa matendo yake malipo mema ya Akhera, Akatekeleza haki za Mwenyezi Mungu na Akatoa katika kulingania Dini, tutamuongezea wema katika matendo yake, tumzidishie thawabu za jema moja mara kumi mpaka kipimo anachokitaka Mwenyezi Mungu cha nyongeza. Na yoyote yule Anayetaka kwa matendo yake ulimwengu peke yake, tutampa tulichomgawia cha huo ulimwengu , na hatakuwa na thawabu zozote huko Akhera.