Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ash-Shuura 42:33

42:33
ان يشا يسكن الريح فيظللن رواكد على ظهره ان في ذالك لايات لكل صبار شكور ٣٣
إِن يَشَأْ يُسْكِنِ ٱلرِّيحَ فَيَظْلَلْنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهْرِهِۦٓ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍۢ لِّكُلِّ صَبَّارٍۢ شَكُورٍ ٣٣
إِن
يَشَأۡ
يُسۡكِنِ
ٱلرِّيحَ
فَيَظۡلَلۡنَ
رَوَاكِدَ
عَلَىٰ
ظَهۡرِهِۦٓۚ
إِنَّ
فِي
ذَٰلِكَ
لَأٓيَٰتٖ
لِّكُلِّ
صَبَّارٖ
شَكُورٍ
٣٣
Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Anapotaka Mwenyezi Mungu Anautuliza upepo, na majahazi yakawa ni yenye kutulia juu ya mgongo wa bahari na kutotembea. Hakika katika kutembea majahazi haya na kusimama kwake baharini kwa uweza wa Mwenyezi Mungu pana mawaidha na hoja waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu, kwa kila mwingi wa uvumilivu juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, kujiepusha na vitendo vya kumuasi na kukubali makadirio Yake, mwingi wa shukrani wa neema Zake na mema Yake.