At-Tawba 9:11 فان تابوا واقاموا الصلاة واتوا الزكاة فاخوانكم في الدين ونفصل الايات لقوم يعلمون ١١
فَإِن
تَابُواْ
وَأَقَامُواْ
ٱلصَّلَوٰةَ
وَءَاتَوُاْ
ٱلزَّكَوٰةَ
فَإِخۡوَٰنُكُمۡ
فِي
ٱلدِّينِۗ
وَنُفَصِّلُ
ٱلۡأٓيَٰتِ
لِقَوۡمٖ
يَعۡلَمُونَ
١١
Basi wakitubu na wakashika Swala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazichambua Aya kwa watu wajuao. 1
Soma Tafsir
Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis
Na iwapo watakomeka na ibada ya asiyekuwa Mwenyezi mungu, wakalitamka neno la kumpwekesha, wakajilazimisha na sheria za Kiislamu za kusimamisha Swala na kutoa Zaka, basi hao ni ndugu zenu katika Uislamu. Na tunazieleza waziwazi aya na kuzifafanua kwa watu wenye kufaidika nazo.
Na iwapo watakomeka na ibada ya asiyekuwa Mwenyezi mungu, wakalitamka neno la kumpwekesha, wakajilazimisha na sheria za Kiislamu za kusimamisha Swala …