Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
9:103
خذ من اموالهم صدقة تطهرهم وتزكيهم بها وصل عليهم ان صلاتك سكن لهم والله سميع عليم ١٠٣
خُذْ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ صَدَقَةًۭ تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٌۭ لَّهُمْ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ١٠٣
خُذۡ
مِنۡ
أَمۡوَٰلِهِمۡ
صَدَقَةٗ
تُطَهِّرُهُمۡ
وَتُزَكِّيهِم
بِهَا
وَصَلِّ
عَلَيۡهِمۡۖ
إِنَّ
صَلَوٰتَكَ
سَكَنٞ
لَّهُمۡۗ
وَٱللَّهُ
سَمِيعٌ
عَلِيمٌ
١٠٣
Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Chukua, ewe Mtume, kwenye mali za hawa waliotubia, waliochanganya matendo mema na matendo mengine maovu, sadaka itakayowasafisha wao na uchafu wa madhambi yao na itakayowainua wao na kuwaondoa kwenye daraja za wanafiki kuwapeleka kwenye daraja za wenye ikhlasi; na watakie wao msamaha wa madhambi yao na uwaombee sitara ya hayo, kwani maombi yako na utakaji msamaha wako ni rehema na utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa kila maombi na kila neno, ni Mjuzi wa hali za waja Wake na nia zao, na Atamlipa kila mwenye kutenda kwa matendo aliyoyatenda.