Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwahisabu watu kuwa wamepotea baada ya kwisha waongoza mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na Mwenyezi mungu Hakuwa ni Mwenye kuwapoteza watu baada ya kuwapa neema uongofu na taufiki, mpaka awaelezee waziwazi yale ambayo yatawapelekea kumcha Yeye na yale wanayoyahitajia ya misingi ya Dini na tagaa zake. Hakika Mwenyezi Mungu, kwa kila jambo, ni Mjuzi; Amewafundisha nyinyi yale ambayo hamkuwa mkiyajua, amewaelezea waziwazi yale ambayo mtanufaika nayo na Amewasimamishia hoja kwa kuwafikishia ujumbe Wake.