Na miongoni mwao wapo walio muahidi Mwenyezi Mungu kwa kusema: Akitupa katika fadhila yake hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika watendao mema. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na miongoni mwa mafukara wa wanafiki, kuna wanaojipa ahadi ya mkazo wenyewe kwamba lau Mwenyezi Mungu Atampa mali, atayatolea sadaka, atafanya vile watu wema wanafanya katika mali yao na atafuata njia ya wema.