Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
052

At-Tur 52:31 قل تربصوا فاني معكم من المتربصين ٣١

52:31
قُلۡ
تَرَبَّصُواْ
فَإِنِّي
مَعَكُم
مِّنَ
ٱلۡمُتَرَبِّصِينَ
٣١
Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia. 1
Endelea Kusoma

Soma Tafsir

Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis

Waambie, «Yangojeeni mauti yangu, kwani mimi pamoja na nyinyi ni katika wenye kuingojea adhabu yenu, na mtaona ni nani atakayekuwa na mwisho mwema.
Zaidi Tafsir

Soma Maudhui Yanayohusiana

Sura 52, Ukurasa 524, Juzuu 27

29. Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu. 30. Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari. 31. Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia. 32. Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu? 33. Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini! 34. Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli. 35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? 36. Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. 37. Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka? 38. Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi! 39. Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana? 40. Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama? 41. Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika? 42. Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka. 43. Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye. 44. Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana. 45. Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa. 46. Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa. 47. Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui. 48. Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama, 49. Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota.

- Swahili Translation - Ali Muhsin Al-Barwani

Maelezo na Tafakari

Hakuna tafakari zilizokaguliwa kwa aya hii

Notes placeholders

Endelea Kuungana na Qur'ani ❤️

Vikumbusho vifupi vyenye maana vinavyoweka upya maisha yako, kukusaidia kutafakari na kuendelea kushikamana na Qur'ani.

Soma, Sikiliza, Tafuta, na Tafakari Qur'ani

Quran.com ni jukwaa linaloaminika na linalotumiwa na mamilioni duniani kote kusoma, kutafuta, kusikiliza na kutafakari kuhusu Qur'ani katika lugha tofauti. Inatoa huduma za tarjuma, tafsiri, vikariri, tarjuma ya neno kwa neno, na zana za ufahamu wa kina, kuifanya Qur'ani ipatikane na kila mtu.

Kama mbinu ya Sadaqah Jariyah, Quran.com imejitolea kusaidia watu kuunganishwa kwa kina na Qur'ani. Ikiungwa mkono na Quran.Foundation , shirika lisilo la faida la 501(c)(3), Quran.com inaendelea kukua kama rasilimali ya bila malipo na yenye thamani kwa wote, Alhamdulillah.

Chunguza
Nyumbani
Redio ya Qur'ani
Wasomaji
Kutuhusu
Watengenezaji
Sasisho za Bidhaa
Maoni
Msaada
Changia
Miradi Yetu
Quran.com
Quran For Android
Quran iOS
QuranReflect.com
Quran.AI
Sunnah.com
Nuqayah.com
Legacy.Quran.com
Corpus.Quran.com
Miradi isiyo ya faida inayomilikiwa, kusimamiwa, au kufadhiliwa na Quran.Foundation
Viungo Maarufu
Dua kutoka Quran
Aya ya Quran ya Siku
Ayatul Kursi
Yaseen
Al Mulk
Ar-Rahman
Al Waqi'ah
Al Kahf
Al Muzzammil
Ramani ya tovutiFaraghaSheria na Masharti
© 2026 Quran.com. Haki Zote Zimehifadhiwa
Changia