Az-Zumar 39:23 الله نزل احسن الحديث كتابا متشابها مثاني تقشعر منه جلود الذين يخشون ربهم ثم تلين جلودهم وقلوبهم الى ذكر الله ذالك هدى الله يهدي به من يشاء ومن يضلل الله فما له من هاد ٢٣
ٱللَّهُ
نَزَّلَ
أَحۡسَنَ
ٱلۡحَدِيثِ
كِتَٰبٗا
مُّتَشَٰبِهٗا
مَّثَانِيَ
تَقۡشَعِرُّ
مِنۡهُ
جُلُودُ
ٱلَّذِينَ
يَخۡشَوۡنَ
رَبَّهُمۡ
ثُمَّ
تَلِينُ
جُلُودُهُمۡ
وَقُلُوبُهُمۡ
إِلَىٰ
ذِكۡرِ
ٱللَّهِۚ
ذَٰلِكَ
هُدَى
ٱللَّهِ
يَهۡدِي
بِهِۦ
مَن
يَشَآءُۚ
وَمَن
يُضۡلِلِ
ٱللَّهُ
فَمَا
لَهُۥ
مِنۡ
هَادٍ
٢٣
Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa. 1
Soma Tafsir
Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr and Sheikh Nasir Khamis
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Aliteremsha Mazungumzo mazuri zaidi kuliko yote, nayo ni Qur’ani tukufu, inayofanana katika uzuri wake, upangikaji wake na kutotafautiana kwake, ndani yake mna hadithi, hukumu, hoja na dalili zilizo wazi. Kusomwa kwake kunarudiwa na ule wingi wa kuikariri hauifanyi ichoke…
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Aliteremsha Mazungumzo mazuri zaidi kuliko yote, nayo ni Qur’ani tukufu, inayofanana katika uzuri wake, upangikaji wake na…