Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Enyi watu, kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, iliyoko kwenye ardhi, ile ambayo Amewahalalishia nyinyi, nayo ni iliyo tohara isiyokuwa najisi, inayonufaisha isiyodhuru wala msifuate njia za Shetani katika kuhalalisha, kuharamisha, uzushi na maasia. Hakika Yeye ni adui yenu mwenye uadui uliyo wazi.