Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
2:223
نساوكم حرث لكم فاتوا حرثكم انى شيتم وقدموا لانفسكم واتقوا الله واعلموا انكم ملاقوه وبشر المومنين ٢٢٣
نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌۭ لَّكُمْ فَأْتُوا۟ حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا۟ لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُم مُّلَـٰقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٢٢٣
نِسَآؤُكُمۡ
حَرۡثٞ
لَّكُمۡ
فَأۡتُواْ
حَرۡثَكُمۡ
أَنَّىٰ
شِئۡتُمۡۖ
وَقَدِّمُواْ
لِأَنفُسِكُمۡۚ
وَٱتَّقُواْ
ٱللَّهَ
وَٱعۡلَمُوٓاْ
أَنَّكُم
مُّلَٰقُوهُۗ
وَبَشِّرِ
ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
٢٢٣
Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana naye. Na wape bishara njema Waumini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Wake zenu ni pahali pa makulima yenu, mnaweka tone la manii ndani ya uzao wao, wakatoka humo watoto kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, waingilieni pale pahali pake pa kuingiliwa tu, napo ni tupu ya mbele, kwa namna yoyote mtakayo. Na zitangulizieni nafsi zenu amali njema kwa kuzitunga amri za Mwenyezi Mungu. Na muogopeni Mwenyezi Mungu na mjue kwamba mtakutana na Yeye kwa kuhesabiwe Siku ya Kiyama. Na wape bishara njema Waumini, ewe Nabii, kwa yale ambayo yatawafurahisha na kuwapendeza ya malipo mema huko Akhera.