Na itakapo kwisha Swala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Basi mkisha kuisikia hutuba na mkaitekeleza Swala, tawanyikeni kwenye ardhi na mtafute riziki ya Mwenyezi Mungu kwa kwenda mbio kwenu, na mtajeni Mwenyezi Mungu kwa wingi katika hali zenu zote, ili mfaulu kuzipata kheri mbili: za duniani na za Akhera.