Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
2:136
قولوا امنا بالله وما انزل الينا وما انزل الى ابراهيم واسماعيل واسحاق ويعقوب والاسباط وما اوتي موسى وعيسى وما اوتي النبيون من ربهم لا نفرق بين احد منهم ونحن له مسلمون ١٣٦
قُولُوٓا۟ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَآ أُنزِلَ إِلَىٰٓ إِبْرَٰهِـۧمَ وَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ وَٱلْأَسْبَاطِ وَمَآ أُوتِىَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَآ أُوتِىَ ٱلنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍۢ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُۥ مُسْلِمُونَ ١٣٦
قُولُوٓاْ
ءَامَنَّا
بِٱللَّهِ
وَمَآ
أُنزِلَ
إِلَيۡنَا
وَمَآ
أُنزِلَ
إِلَىٰٓ
إِبۡرَٰهِـۧمَ
وَإِسۡمَٰعِيلَ
وَإِسۡحَٰقَ
وَيَعۡقُوبَ
وَٱلۡأَسۡبَاطِ
وَمَآ
أُوتِيَ
مُوسَىٰ
وَعِيسَىٰ
وَمَآ
أُوتِيَ
ٱلنَّبِيُّونَ
مِن
رَّبِّهِمۡ
لَا
نُفَرِّقُ
بَيۡنَ
أَحَدٖ
مِّنۡهُمۡ
وَنَحۡنُ
لَهُۥ
مُسۡلِمُونَ
١٣٦
Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Semeni, enyi Waumini, kuwaambia Mayahudi na Wanaswara, “Tumemuamini Mwenyezi Mungu, Aliye Mmoja, Anayeabudiwa kwa haki; na tumeiamini Qur’ani tuliyoteremshiwa ambayo Mwenyezi Mungu alimletea Wahyi Nabii wake na Mtume Wake Muhammad, rehema na amani zimshukie; na tumeziamini Kurasa alizoteremshiwa Ibrāhīm na watoto wake wawili: Ismāīl na Is’ḥāq, na alizoteremshiwa Ya’qūb na Asbāṭ - Manabii wanaotokana na watoto wa Ya’qūb waliokuwa katika makabila kumi na mbili ya Wana wa Isrāīl-; na tumeiamini Taurati aliyopewa Mūsā na Injil aliyopewa Īsā na Wahyi ulioteremshwa kwa Mitume wote. Hatumbagui yoyote miongoni mwao katika kuamini. Na sisi ni wenye kumdhalilikia Mwenyezi Mungu kwa kumtii na kumuabudu.”