Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Wakiyaamini Makafiri, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara na wengineo, kama yale milyoyaamini nyinyi katika yale aliyokuja nayo Mtume, basi wameongoka kwenye haki; na wakikataa, basi wao wako kwenye upinzani mkubwa. Mwenyezi Mungu Atakutosheleza, ewe Mtume, shari lao na Atakupa ushindi juu yao. Yeye Ndiye Msikizi wa maneno yenu, Ndiye Mjuzi wa hali zenu.