Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na ukiogopa, ewe Mtume, hiana ambayo ishara zake zimejitokeza, kutoka kwa kundi lolote, basi watupilie mbali ahadi yao, ili zote pande mbili ziwe zimelingana kwa kujua kwamba hapana tena mapatano baada ya leo. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kuenda kinyume na ahadi zao, wavunjaji ahadi na mapatano.