Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha
9:90
وجاء المعذرون من الاعراب ليوذن لهم وقعد الذين كذبوا الله ورسوله سيصيب الذين كفروا منهم عذاب اليم ٩٠
وَجَآءَ ٱلْمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ ۚ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌۭ ٩٠
وَجَآءَ
ٱلۡمُعَذِّرُونَ
مِنَ
ٱلۡأَعۡرَابِ
لِيُؤۡذَنَ
لَهُمۡ
وَقَعَدَ
ٱلَّذِينَ
كَذَبُواْ
ٱللَّهَ
وَرَسُولَهُۥۚ
سَيُصِيبُ
ٱلَّذِينَ
كَفَرُواْ
مِنۡهُمۡ
عَذَابٌ
أَلِيمٞ
٩٠
Na walikuja wenye kutoa udhuru katika Mabedui ili wapewe ruhusa, na wakakaa wale walio mwambia Mwenyezi Mungu na Mtume wake uwongo. Itawafika walio kufuru katika wao adhabu chungu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Na kilikuja kikundi, miongoni mwa watu wa vitongoji vya Waarabu wa majangwani, kandokando ya mji wa Madina wakitoa nyudhuru kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, wakimuelezea udhaifu walionao na kutoweza kwao kutoka kwenda vitani. Na kuna watu waliojikalia bila kutoa udhuru wowote kwa kumfanyia ujasiri Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema wa Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Basi wale waliokufuru miongoni mwa hawa itawatapata adhabu kali, ya kuuawa na nyinginezo hapa duniani, na ya Moto kesho Akhera.