Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Aya Zinazohusiana
Na tukawawekea nyinyi humo vitu mnavyovihitajia katika maisha yenu miongoni mwa makulima, wanyama, aina mbalimbali ya shughuli za kujipatia maisha na vinginevyo. Na tukawaumbia nyinyi watoto, watumishi na wanyama manaonufaika nao. Na riziki zao haziko juu yenu, bali ziko juu ya Mwenyezi Mungu Bwana wa viumbe vyote kwa wema utokao Kwake na ukarimu.