Na ndio kama hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata miji inapo kuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kama nilivyowapatiliza kwa adhabu watu wa miji iliyodhulumu kwa kuenda kinyume na amri yangu na kuwakanusha Mitume wangu, nitawapatiliza wengineo miongoni mwa watu wa miji wakizidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumuasi Yeye na kuwakanusha Mitume Wake. Hakika mapatilizo Yake ya mateso ni makali, yenye kuumiza, yaliyo magumu.