Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda apendavyo. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Watakuwa ni wenye kukaa humo milele muda wa kuweko mbingu na ardhi, hivyo basi adhabu yao haitakatika wala haitakoma, bali ni adhabu ya daima iliyotiliwa mkazo, isipokuwa iwapo Mola wako atataka, kwa kuwatoa waliompwekesha waliofanya maasia baada ya muda fulani wa kukaa kwao Motoni. Hakika Mola wako ni Mwenye kufanya Analolitaka.