Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Hud 11:43

11:43
قال ساوي الى جبل يعصمني من الماء قال لا عاصم اليوم من امر الله الا من رحم وحال بينهما الموج فكان من المغرقين ٤٣
قَالَ سَـَٔاوِىٓ إِلَىٰ جَبَلٍۢ يَعْصِمُنِى مِنَ ٱلْمَآءِ ۚ قَالَ لَا عَاصِمَ ٱلْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ ٱللَّهِ إِلَّا مَن رَّحِمَ ۚ وَحَالَ بَيْنَهُمَا ٱلْمَوْجُ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُغْرَقِينَ ٤٣
قَالَ
سَـَٔاوِيٓ
إِلَىٰ
جَبَلٖ
يَعۡصِمُنِي
مِنَ
ٱلۡمَآءِۚ
قَالَ
لَا
عَاصِمَ
ٱلۡيَوۡمَ
مِنۡ
أَمۡرِ
ٱللَّهِ
إِلَّا
مَن
رَّحِمَۚ
وَحَالَ
بَيۡنَهُمَا
ٱلۡمَوۡجُ
فَكَانَ
مِنَ
ٱلۡمُغۡرَقِينَ
٤٣
Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji. (Nuhu) akasema: Leo hapana wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu ila aliye mrehemu mwenyewe. Na wimbi likawatenganisha, akawa katika walio zama. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mtoto wa Nūḥ akasema, «Nitakimbilia kwenye jabali nijihifadhi na maji na hilo litanizuia na kuzama. Nūḥ akamjibu, «Leo hakuna kitu chenye kuzuia amri ya Mwenyezi Mungu na hukumu Yake iliyoteremka kwa viumbe, ya gharika na maangamivu, isipokuwa yule aliyehurumiwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, basi amini na upande jahazini pamoja na sisi.» Hapo mawimbi makubwa yalitenganisha baina ya Nūḥ na mwanawe na akawa ni miongoni mwa waliogharikishwa wenye kuangamia.