Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ibrahim 14:10

14:10
۞ قالت رسلهم افي الله شك فاطر السماوات والارض يدعوكم ليغفر لكم من ذنوبكم ويوخركم الى اجل مسمى قالوا ان انتم الا بشر مثلنا تريدون ان تصدونا عما كان يعبد اباونا فاتونا بسلطان مبين ١٠
۞ قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِى ٱللَّهِ شَكٌّۭ فَاطِرِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍۢ مُّسَمًّۭى ۚ قَالُوٓا۟ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌۭ مِّثْلُنَا تُرِيدُونَ أَن تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ ءَابَآؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَـٰنٍۢ مُّبِينٍۢ ١٠
۞ قَالَتۡ
رُسُلُهُمۡ
أَفِي
ٱللَّهِ
شَكّٞ
فَاطِرِ
ٱلسَّمَٰوَٰتِ
وَٱلۡأَرۡضِۖ
يَدۡعُوكُمۡ
لِيَغۡفِرَ
لَكُم
مِّن
ذُنُوبِكُمۡ
وَيُؤَخِّرَكُمۡ
إِلَىٰٓ
أَجَلٖ
مُّسَمّٗىۚ
قَالُوٓاْ
إِنۡ
أَنتُمۡ
إِلَّا
بَشَرٞ
مِّثۡلُنَا
تُرِيدُونَ
أَن
تَصُدُّونَا
عَمَّا
كَانَ
يَعۡبُدُ
ءَابَآؤُنَا
فَأۡتُونَا
بِسُلۡطَٰنٖ
مُّبِينٖ
١٠
Mitume wao wakasema: Ati pana shaka na Mwenyezi Mungu, Muumba mbingu na ardhi? Yeye anakuiteni apate kukufutieni madhambi yenu, na akupeni muhula mpaka muda ulio wekwa. Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni wanaadamu kama sisi. Mnataka kutuzuilia na waliyo kuwa wakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni hoja ilio wazi. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mitume wao wakasema kuwaambia, «Je, pana shaka yoyote juu ya Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye Ndiye Muabudiwa Peke Yake, na hali Yeye ni Muumba wa mbingu na ardhi na Mwenye kuzifanya zipatikane kutoka kwenye hali ya kutokuwako bila ya kuwa na mfano uliotangulia, na hali Yeye Anawaita kwenye Imani Apate kuwasamehe mliyoyatanguliza ya ushirikina na Awaepushie adhabu ya kumaliza kabisa, Awape nafasi ya kusalia ulimwenguni mpaka muda Aliyoupanga ambao ni kikomo cha nyakati za maisha yenu, Asiwaadhibu duniani? Wakawaambia Mitume wao, «Hatuwaoni nyinyi isipokuwa ni binadamu, hali zenu ni kama zetu, hamna ubora wowote juu yetu wa kuwafanya muwe Mitume. Mnataka kutuzuia kuviabudu vitu ambavyo baba zetu walikuwa wakiviabudu miongoni mwa masanamu na mizimu. Basi tuletee hoja iliyo wazi yenye kuonyesha usahihi wa yale mnayoyasema.