Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Ibrahim 14:11

14:11
قالت لهم رسلهم ان نحن الا بشر مثلكم ولاكن الله يمن على من يشاء من عباده وما كان لنا ان ناتيكم بسلطان الا باذن الله وعلى الله فليتوكل المومنون ١١
قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِن نَّحْنُ إِلَّا بَشَرٌۭ مِّثْلُكُمْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ ۖ وَمَا كَانَ لَنَآ أَن نَّأْتِيَكُم بِسُلْطَـٰنٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ ١١
قَالَتۡ
لَهُمۡ
رُسُلُهُمۡ
إِن
نَّحۡنُ
إِلَّا
بَشَرٞ
مِّثۡلُكُمۡ
وَلَٰكِنَّ
ٱللَّهَ
يَمُنُّ
عَلَىٰ
مَن
يَشَآءُ
مِنۡ
عِبَادِهِۦۖ
وَمَا
كَانَ
لَنَآ
أَن
نَّأۡتِيَكُم
بِسُلۡطَٰنٍ
إِلَّا
بِإِذۡنِ
ٱللَّهِۚ
وَعَلَى
ٱللَّهِ
فَلۡيَتَوَكَّلِ
ٱلۡمُؤۡمِنُونَ
١١
Mitume wao wakawaambia: Sisi kweli si chochote ila ni wanaadamu kama nyinyi. Lakini Mwenyezi Mungu humfanyia hisani amtakaye katika waja wake. Wala sisi hatuwezi kuleta uthibitisho ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu ndio wategemee Waumini. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Mitume waliposikia yale yaliyosemwa na watu wao waliwaambia, «Ni kweli kwamba sisi hatukuwa isipokuwa ni binadamu kama nyinyi, kama mlivyosema. Lakini Mwenyezi Mungu Anawafanyia wema Anaowataka miongoni mwa waja wake kwa kuwapa neema Zake na kuwateua kwa kuwapa utume Wake. Na hizo dalili waziwazi mlizozitaka, haiwezekani sisi kuwaletea isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na taufiki Yake. Na kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake wanategemea Waumini katika mambo yao yote.