Kinamtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo katika mbingu na katika ardhi. Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake. Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadithi
Vinamtakasa Mwenyezi Mungu na sifa zisizonasibiana na Yeye vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini. Ni Wake Yeye Mwenyezi Mungu, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, uendeshaji mambo usio na kizuizi katika kila kitu. Na Yeye Ndiye Mwenye sifa njema zilizo nzuri. Na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.