Na anaye kufuru, isikuhuzunishe kufuru yake. Kwetu ndio marudio yao, na hapo tutawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mwenye kukanusha, usimsikitikie, ewe Mtume, wala usiwe na huzuni, kwa kuwa wewe umetekeleza wajibu wako wa ulinganizi na ufikishaji, kwetu sisi ndio marejeo yao na mwisho wao Siku ya Kiyama, tuwapashe habari ya matendo yao maovu waliyoyafanya duniani, kisha tuwalipe kwa hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yale ambayo nyoyo zao zinayaficha, ya kumkanusha Mwenyezi Mungu na kufadhilisha kumtii Shetani.